AfyaHabari

Rais aongoza maafisa wakuu kupewa chanjo ya covid 19……

Rais Uhuru Kenyatta leo ameongoza maafisa wakuu wa serikali kupokea chanjo ya corona katika Ikulu ya Nairobi.

Baada ya kutangaza masharti mapya ya kupambana na ongezeko la visa vya Covid 19 nchini, rais alikuwa wa kwanza kuchanjwa kisha mkewe Margaret Kenyatta akapewa chanjo hiyo.

Miongoni mwa mawaziri waliopokea chanjo hiyo ni pamoja na waziri wa usalama wa ndani Daktari  Fred Matiang’I,waziri wa afya Mutahi Kagwe na waziri wa mabo ya nje Racheal Omamo ,kaimu Jaji mkuu Philomena Mwilu na viongozi mbalimbali wakiwemo wa kidini.

Hapo awali Rais Kenyatta aliwaagiza mawaziri na makatibu wote kuchanjwa dhidi ya corona.

Wakati huo huo rais Kenyatta amewahimiza wakenya haswa vijana kufuata masharti ya covid 19 akisema ugonjwa huo unasababisha vifo.

Amewahimizi wananchi kukubali kuchanjwa ili kuokoa maisha ya wengi.

Aidha rais amesema wale wote wanaoingia humu nchini kutoka mataifa ya nje lazima wawe na cheti cha kuthibitisha hawana corona.