HabariLifestyle

WAFANYA BIASHARA MALINDI WAKERWA NA DENI

Wafanyibiashara katika soko jipya mjini Malindi kaunti ya Kilifi sasa wanalalamikia kulimbikiziwa madeni na Manispaa mji huo Wakidai madeni hayo yaliachwa na waliowahi kufanyabiashara sokoni humo.

Wakiongozwa na Kadzo Phillip wanasema wameshangaa kwanini usimamizi wa soko hilo umekuwa ukiwawekea madeni ambayo yanafaa kulipwa na wafanyibiashara walioacha kuendelea na biashara zao sokoni humo.

Wanyibiashara hao wanadai Manispaa mjini Malindi imetishia kuwapeleka mahakamani endapo watashindwa kulipa madeni hayo.

Hata hivyo, Afisa Msimamizi wa Manispaa ya Malindi Julius Fondo amekanusha madai hayo akisema wamekuwa wakifuatilia wanaofaa kulipa madeni hayo na kusisitiza hakuna mfanyibiashara analimbikiziwa deni asilolifahamu.