Habari

Magoha alalamikia kukithiri kwa udanganyifu katika mtihani wa KCSE kupitia njia ya simu……

Waziri wa elimu Professor George Magoha amelalamikia kukithiri kwa udanganyifu wa mtihani wa kitaifa wa KCSE kupitia njia ya simu.

Akizungumza katika kaunti ya Homa Bay mapema leo , Magoha amesema watu kadhaa tayari wamekatwa kuhusiana na visa hivi akiwaonya vikali kuwa wapelelezi wakue macho kuwakabili washukiwa zaidi.

Tayari watu 13 wakiwemo walimu na wanafunzi kaunti ya Nyamira pekee wamepelekwa mahakamani hii leo baada ya kukamatwa kutokana na wizi wa mtihani huo.