AfyaHabariSiasa

Kalonzo Musyoka ahimiza wakenya wote kuchanjwa….

Kinara wa chama cha WIPER Kalonzo Musyoka amesisitiza umuhimu wa wakenya wote kuchanjwa ili kuzuia kuambukizwa virusi vya corona.

Akizungumza katika hafla ya mazishi ya mfanyibiashara Peter Kanyi mjini Machakos,Kalonzo amepuzilia mbali propaganda zinazoenezwa mitandaoni kuhusu chanjo hii akisema maafisa wa utafiti wameithibitisha kuwa salama huku akiwashauri wakenya kutohofu.

Kalonzo pia amempongeza rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, baada ya kuruhusu utafiti wa kisayansi kuhusu maambukizi ya Corona kufanywa nchini humo, tofauti na mtangulizi wake hayati Magufuli aliyepinga hitaji hilo.