Habari

Waumini wa dini ya kiislamu wajiandaa kuupokea mwezi mtukufu wa ramadhan…

Waislamu katika eneo la Tana Delta kaunti ya Tana River wametakiwa kufuata kanuni za wizara ya afya ya kudhibiti msambao wa virusi vya corona wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Sheikh Abdullahi Bakero ambae pia ni imamu wa msikiti jamia mjini Garsen amewasihi waislamu kuendelea kufuata sheria hizo wakati wanapoendelea na ibada haswa nyakati za usiku ili kujikinga na mambukizi ya virusi vya covid-19.

Vile vile amewasihi wale wanaojiweza katika jamii kuwapa msaada wale wa chini wakati wa Ramadhan huku akisema watu wengi wameathirika kiuchumi kutokana na masharti ya corona yaliyowekwa na serikali.

Hapa mjini Mombasa waumini wa dini ya kiislamu wameendelea kuishinikiza serikali kupunguza muda wa kutokuwa nje ili kuwapatia muda zaidi kutekeleza ibada.

Waumini hao wanatarajiwa kutizama mwezi leo jioni na iwapo mwezi utaandama basi mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan utaanza leo.