HabariSiasa

Mohammed Abdulqadir Haji aapishwa kuwa seneta wa Garissa…

Seneta mteule wa kaunti ya Garissa Mohammed Abdulqadir Haji ameapishwa rasmi kuwa seneta wa kaunti hiyo katika majengo ya bunge la seneti.

Haji alitangazwa kuwa seneta wa Garissa bila ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo baada ya kukosa mpinzani wake.

Alichaguliwa na chama cha JUBILEE kujaza nafasi hiyo baada ya aliyekuwa seneta marehemu babake Yusuf Haji kufariki dunia mwezi februari mwaka huu.

Maseneta wakiongozwa na Kipchumba Murkomen wamempongeza seneta Haji kwa kuchaguliwa bila kupingwa huku wakimuhimiza kuendeleza kazi ilioachwa na babake.

Haji alisifiwa kwa juhudi zake za kuwaokoa wakenya wakati wa mkasa wa shambulizi la jumba la kibiashara la Westgate mnamo mwaka 2013.