Habari

Mwanahabari wa KBC Betty Barasa aliyeuawa kwa kuzikwa leo……

Mwanahabari wa shirika la KBC Betty Barasa aliyeuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake mtaani Ngong anazikwa leo katika boma lake eneo la Ololua, Ngong.

Betty aliuawa siku ya Jumatano usiku wiki iliyopita kwa kupigwa risasi nyumbani kwake na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki.

Marehemu alikuwa mhariri wa video katika idhaa ya kitaifa KBC na alivamiwa na watu waliokuwa wamemngojea punde tu alipowasili nyumbani kwake mwendo wa saa mbili unusu jioni kutoka kazini.

Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini kilichopelekea mauaji ya mwanahabari huyo kwa sababu wauaji wake waliiba tu simu na tarakilishi kabla ya kutoroka.