Habari

Shule kufanyiwa ukaguzi kabla ya kufunguliwa mwezi Mei…..

Waziri wa Elimu proffesa George Magoha ameagiza ukaguzi wa shule kuhakikisha kanuni za usalama za COVID 19 zinazingatiwa kabla ya kufunguliwa kwa shule ifikapo tarehe 10 ya mwezi ujao wa 10.

Waziri Magoha amepinga uwezekano wa kurekebisha kalenda ya shule, akitoa mfano wa kubanwa kwa maambukizo ya Covid lakini akasisitiza kuwa wataendelea kuchunguza na kuongozwa na safu ya maambukizo ya Covid-19.

wakati huo huo Magoha amesema kuwa usahihishaji wa mtihani wa kidato cha nne KCSE unakusudiwa kuanza majuma matatu yajayo.

Akizungumza katika eneo la Naivasha Magoha amesema kuwa swala la usalama limepewa kipaumbele akiongeza kuwa walimu wote ambao watahusika katika zoezi hili lazma wapate chanjo ya Covid 19 .

Magoha aidha amesema swala la usafiri wa wanafunzi wa kidato cha nne linashughulikiwa kuhakikisha kila mwanafunzi anafika nyumbani salama haswa wanaotoka kaunti tano zilizositishwa usafiri.