Habari

Wakili Philip Murgor akabiliwa na wakati mgumu mbele ya jopo la JSC……..

Zoezi la kumteua jaji mkuu limeingia siku ya tano hii leo ikiwa ni zamu ya wakili Philip Murgor kuhojiwa na ambaye amejipata pabaya wakati wa kujibu maswali ya kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu, alipodai kwamba kuna pengo katika utendakazi wa mahakama wakti huu ambapo hamna jaji mkuu.

 

Mwilu amemtaka Murgor kufafanua iwapo anamaanisha kwamba kaimu jaji mkuu ambaye ni yeye kwa sasa hanauwezo wa kutekeleza majukumu hayo.

 

Wawili hao aidha wamaonekana kukwaruzana zaidi wakti wa  majohiano hayo.

 

Hata hivyo tatizo la majaji wa kutosha kwenye idara ya mahakama limejitokeza tena huku Murgor akisema iwapo ataidhinishwa kuwa jaji mkuu atahakikisha kuwa majaji 41 ambao hawajahapishwa hadi sasa licha ya majina yao kuwakilishwa kwa rais Uhuru Kenyatta wanaapishwa.

 

Murgor aidha ameongeza kuwa swala lingine linalolemeza idara hiyo ni ukosefu wa fedha.

 

Wagombeaji wa tano wa kuwania wadhfa huo wa jaji mkuu watahojiwa wiki ijayo.