Habari

Wafugaji wa ngombe wa maziwa kwenye eneo la bamba kaunti ya kilifi ni miongoni mwa eneo lililoathirika na ukame…

Wafugaji wa ngombe wa maziwa  kwenye eneo la bamba kaunti ya kilifi ni miongoni mwa eneo lililoathirika na ukame unaoendelea kushuhudiwa kwenye maeneo mbali mbali nchini.

Ilivyo sasa mifugo wanakosa maji na chakula jambo ambalo limesababisha ngombe wengi kutotoa maziwa na jumuiya ya  ushirika wa biashara eneo hilo limenakili kupungua kwa wanachama wake kwa asilimia kubwa zaidi.

Takwimu inaonyesha kwamba ni wakulima kumi pekee ambao wanaendeleza shughuli ya usambazaji maziwa ikilinganishwa na wanachama ambao ni 158.

Bamba ni miongoni mwa maeneo mwa kilifi ambayo yanakumbwa na makali ya mabadiliko ya hali ya anga vijiji vya vikwatani,mwanamwinga,kayafungo na kajongoni kwenye eneo la kaloleni pia vimeathiriwa pakubwa na mabadiliko hayo.