Habari

Wanafunzi waliomaliza KCSE katika kaunti tano zilizofungwa watatizika na usafiri…

Wanafunzi waliomaliza mtihani wa KCSE wamelala katika bustani ya Uhuru Park jijini Nairobi baada ya kushindwa kupata usafiri wa nyumbani kwa sababu ya marufuku ya usafiri inayotekelezwa sasa katika kauti tano humu nchini.

Hii ni baada ya kushindwa kuendelea na safari zao za kuelekea nyumbani baada ya muda wa amri ya kutotoka nje kuwapata wakiwa bado hawajaondoka jijini Nairobi kuelekea makwao walipomaliza kuufanya mtihani wao wa mwisho.

Rais Uhuru Kenyatta alitangaza amri ya kukaa nyumbani katika kaunti 5 ikiwemo Nairobi ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Amri hiyo inatekelezwa ikiambatana na amri ya kutotoka nje usiku kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi alfajiri.

Haya yanajiri huku shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty limeikosoa serikali kwa uamuzi wake wa kuzifunga kaunti hizo tano.