AfyaMakala

Faida Za Kufunga Kula (Fasting) Sehemu ya Kwanza…….

Watu wengi wanafahamu kuwa kufunga kula ni suala linalohusiana na imani za kidini.Ila hawafahamu kuwa kufunga kula kuna manufaa ya kiafya pia.

Ripota wetu amekuandalia makala maalum ya Faida za Kufunga.

Huboresha mzunguko wa damu

Kufunga kula hufanya mzunguko wa damu uende vizuri hasa kwa watu wenye aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari (Type 2 Diabetes). Hata hivyo, auguaye kisukari anashauriwa kupata ushauri wa daktari kufahamu kama kweli anaruhusiwa kufunga au la. Si vizuri mtu kujilazimisha matokeo yakawa ni kujidhoofisha kabisa kiafya.

Husaidia kupunguza uzani

Kufunga kula ni njia mojawapo iliyo bora zaidi kupunguza uzani kwani kwa njia hii, mwili hutumia mafuta yaliyoko mwilini ili kujipa nguvu.

Hupunguza shinikizo la damu

Watu wengi wanapofunga hujikuta pia shinikizo la damu likipungua, hii inasababishwa na kupungua kwa kiwango cha chumvi kwenye damu.

chumvi nyingi husababisha shinikizo la damu. Hivyo kufunga ni kupunguza kiasi cha chumvi kinachoingia mwilini.