HabariSiasa

PSC kuwasilisha majina ya wanajopo wa kuteua makamishna wa IEBC kwa rais….

Tume ya huduma za bunge PSC inatarajiwa kuwasilisha majina ya walioteuliwa kuhudumu katika jopo litakaloteua mahakamishna 4 wa tume ya IEBC kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Kwa mujibu wa sheria watakaohudumu katika jopo hilo ni wanawake 2 na wanaume 2 waliteuliwa na PSC. 1 kutoka kwa chama cha mawakili LSK na 2 kutoka kwa baraza la makanisa nchini.

Rais Uhuru Kenyatta alitangaza nafasi hizo kuwa wazi tarehe 14 mwezi huu ambapo leo ni siku ya 7 na ya mwisho. Aidha Rais  Kenyatta, atahitajika kuchapisha majina hayo  katika gazeti rasmi la serikali ili kupisha mchakato wa mahojiano.