Habari

RAIS UHURU KENYATTA AHIMIZA KUONGEZWA KWA IDADI YA VIJANA WANAOSAJILIWA KWA HUDUMA YA NYS……..

Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wasimamizi wa majeshi  ya ulinzi nchini kuongeza idadi wa vijana wa huduma kwa taifa nchini NYS katika  majeshi ya ulinzi wakati wa kuwatafuta makurutu.

Akizungumza katika hafla ya sherehe za kufuzu kwa  makurutu 7,479 wa shirika  la huduma ya vijana kwa taifa ya NYS mjini Gilgil kaunti ya Nakuru, Rais Kenyatta amesema idadi ya vijana ambao wamekuwa wakisajiliwa ni ya chini ikilinganishwa na ujuzi wanaopokea katika mafunzo.

Ameshabikia utendakazi wa NYS katika ufanisi wa taifa ya kiuchumi na kimaendeleo hasa baada yao kujumuishwa katika mipango muhimu ya kiserikali.

Aidha amepongeza vijana hao sawia na wasimamizi wao kwa kufuzu katika mazingira yaliyojaa changamoto ya janga la Corona bila kuripotiwa kisa hata kimoja.

Kinyume na hapo awali familia za makurutu hao hazikuruhusiwa kuhudhuria hafla hiyo ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.

By News Desk