Habari

BUNGE LA KAUNTI YA TAITA TAVETA LAOMBOLEZA KIFO CHA MWAKILISHI WADI JOYCE MWANGOJI………..

Bunge la kaunti ya  Taita Taveta na wakaazi wa eneo hilo kwa jumla wanaendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa mwakilishi wadi maalum katika kaunti hiyo Joyce  Mwangoji ,Mwangoji amefariki mapema leo katika hospitali St Joseph ilioko mjini voi..

Spika wa mbunge la Taita Taveta  Meshark Maghanga amedhibitisha kufariki kwa mbunge huyo,Maganga amesema  Mwangoji amefariiki akiwa anapelekwa katika hospitali ya St Jospeph Shelter of Hope mjini Voi.

Hadi kifo chake Mwagoji amekuwa akihudumu katika wadhfa wa mwenyekiti wa maendeleo ya wanawake, mwanachama wa sauti ya wanawake na mwanaharakati wa haki za kibinaadam.

Mwangoji ni  kiongozi wa tatu wa kike kufariki akiwa ofisini katika kipindi cha mwaka mmoja,Beatrace Mwabili aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Wundanyi Mbale,  alifariki mwaka jana  baada ya kuugua saratani ,mwaka wa elfu mbili kumi na tisa mwakilishi wadi maalum maarufu Anastancia Wakesho alifariki baada ya kuugua saratani ya matiti ,