Habari

Malezi duni ya watoto TAITA yachangia ukiukaji wa haki za watoto…

 Idara ya watoto katika kaunti ya Taita Taveta imesema kuwa asilimia kubwa ya visa vya ukiujaji wa haki za watoto ni wazazi kutelekeza watoto  ikifuatwa na dhulma za kijinsia.

Mshirikishi wa maswala ya watoto kaunti ya Taita Taveta Juma Boga amesema kuwa visa vya wazazi kutelekeza watoto wao vinaongoza kwa takriban asilimia 60.

Boga amesema kuwa watoto wengi katika kaunti ya Taita Taveta wanalelewa na walezi wazee ambao hawana uwezo wa kimapato kushughulikia mahitaji ya watoto.

Aidha ameongeza kuwa hatua hiyo imechangia watoto wengi kukosa haki zao za kimsingi kama malezi bora, elimu, afya huku wengine wakipitia dhulma za kijinsia.

Afisa huyo kadhalika amewashauri wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao pamoja na kujihusisha katika maswala ya watoto kuhakikisha wanapata haki zote.