Habari

Mkuu wa UNHCR asema Kenya haifungi kambi za wakimbizi…

Serikali ya Kenya haifungi kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma lakini inataka suluhisho, haya ni kulingana na kamishna mkuu wa shirika la wakimbizi laumoja wa mataifa.

Filippo Grandi ameyasema hayo wakati akitembelea DR Congo, Rwanda na Burundi, ili kufahamu shida ambazo zinawakabili wakimbizi katika maeneo hayo.

Mwezi uliopita, Kenya ilitoa makataa ya siku 14 ya kufungwa kambi za Dadaab na Kakuma, ikitoa sababu za hofu ya usalama wa kitaifa, na wizara ya mambo ya ndani ilikuwa imesema “hakuna nafasi ya mazungumzo zaidi”.

Nchini Rwanda Jumapili, Bwana Grandi aliwaambia waandishi wa habari kwamba wamefanya mazungumzo mazuri sana na serikali ya Kenya akisema , serikali ya Kenya inataka kupata suluhisho.

Amesema shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa limewasilisha kwa Kenya mipango ya baadaye ya kambi hizo mbili.

By News Desk