HabariSiasa

Wawaniaji wa wadhfa wa jaji wa mahakama ya upeo waanza kuhojiwa……

Shughuli ya kuwahoji wawaniaji wa wadhifa wa jaji wa mahakama ya upeo imeanza rasmi huku Saidi Chitembwe Juma akiwa wa kwanza kufika mbele ya makamishena wa tume ya huduma za mahakama JSC.

Chitembwe ametakiwa kueleza majukumu makuu ya mahakama ya upeo huku akitakiwa kutoa mfano wa kesi zilizoonyesha uhuru wa mahakama hio.

Kikao hicho, Chitembe ameweka wazi kuhusu msimamo wake wa kupunguza mrundiko wa kesi mahakamani ambao umekuwa changamoto kwenye idara hio ya mahakama kwa muda mrefu.

Aidha, kamishena ambaye ni jaji Mohamed Warsame amemtaka Chitembwe kutoa mfano wa kesi ambazo ziliamuliwa na mahakama hio na ambazo anahisi hazikuzingatia sheria ipasavyo.

By reporter Nicky Waita