HabariLifestyle

Baadhi ya wakaazi Kwale wadinda kuchukua neti za mbu…

Baadhi ya wakaazi katika kaunti ya Kwale wamedinda kuchukua vyandarua vya kuzuia mbu vinavyotolewa bure na serikali ya kaunti hiyo.

Kulingana na afisa mkuu wa afya katika kaunti hio Francis Gwama, wakaazi hao wanadai kwamba neti hizo zina matundu makubwa ya kupitisha mbu na pia kudaiwa kuongea nyakati za usiku huku wakiongezea kwamba neti hizo pia zinasababisha kunguni.

Miaka mitano iliopita, wakaazi wa ukanda wa pwani walidinda kutwaa neti hizo wakitoa sababu sawia na za wakwale huku wakisema kwamba neti hizo zinawakosesha usingizi.

Wengi walionekana wakitumia neti hizo kwa kuvulia samaki, huku wengine wakifugia vifaranga vya kuku .

Wizara ya ilizindua kampeni ya kusambaza neti milioni 15.7 zilizotibiwa katika kaunti 27 ambazo ziko hatarini ya kuambukizwa malaria huku ikilenga wakenya milioni 25.

Neti zipatazo 500,000 zimesambazwa kwa wakaazi wa Kwale.

By Reporter Nick Waita