HabariKimataifaSiasa

Rais Uhuru Kenyatta yuko nchini Djibouti kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Ishamael Omar Guelleh

Rais Uhuru Kenyatta yuko nchini Djibouti kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Ishamael Omar Guelleh

Rais Kenyatta ambaye mwenyekiti wa jumuia ya Muungano wa Afrika Mashariki (EAC) ameandamana na waziri wa masuala ya kigeni wa hapa nchini Raychelle Omamo.

Rais Omar alichukua hatamu ya uongozi mwaka 1999 alipochaguliwa kuwa rais kwa mara ya kwanza.

Rais huyo wenye umri wa miaka 73 ameshinda kiti hicho kwa kura asilimia 97.44 akimshinda mpinzani wa kipekee Zakariah Ismail Farah aliyejinyakulia asilimia 2.48

Itakumbukwa ni wiki hii tu ambapo Rais Kenyatta alihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

BY JOYCE MWENDWA