HabariSiasa

Idadi ndogo ya wapiga kura yashuhudiwa katika uchaguzi mdogo wa Bonchari na Juja…..

Idadi ndogo ya wapiga kura imeshuhudiwa katika vituo vya upigaji kura eneo bunge la Bonchari kaunti ya Kisii wakati uchaguzi mdogo wa eneo hilo ulipoanza rasmi mapema leo asubuhi.

Haya ni kulingana na tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC huku zoezi hilo likianza bila ya kushuhudiwa visa vyovyote vya udanganyifu.

Mgombea wa chama cha UDA Teresa Bitutu tayari amepiga kura yake naye mgombea wa Jubilee Zebedeo Opore pia ameshapiga kura yake.

Wagombea 13 wanawania kiti hicho cha Bonchari ambapo ushindani mkali uko kati ya Paviel Oineke wa ODM, Zebedeo Opore wa Jubilee na Teresa Bitutu wa UDA.

Huyu hapa ni Teresa Bitutu akizungumza baada ya kupiga kura yake.

Mgombea wa kiti hicho cha Bonchari kupitia chama cha ODM Paviel Oineke pia amelalamikia idadi kubwa na maafisa wa polisi wanaosimamia uchaguzi huo.

Akizungumza baada ya kupiga kura yake Oineke amelalamikia kutiWa nguvuni kwa baadhi ya wafuasi wake na maajenti wake huku akiwarai wananchi kujitokeza kwa wingi na kupiga kura.

Kiti cha Bonchari kiliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge John Oyoo OYIOKA.

Wakati huo huo uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Juja ulianza saa kumi na mbili asubuhi huku idadi ya wanaojitokeza kupiga kura kufikia sasa ikiwa ni ndogo mno.

Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kifo cha Francis Waititu Wakapee…

By Reporter Warda Ahmed.