HabariSiasa

Martha Koome aapishwa kuwa jaji mkuu mpya nchini…….

Martha Karambu Koome sasa ndiye jaji mkuu mpya na rais wa mahakama kuu nchini na mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo katika historia ya Kenya.

Jaji Koome ameapishwa rasmi leo katika ikulu ya rais, hafla iliyoongozwa na rais Uhuru Kenyatta.

Akiapishwa Koome ameapa kutekeleza haki katika makujumu yake kulingana na katiba ya Kenya, bila ya mapendeleo.

Wakati huo huo Jaj William Ouko amepishwa rasmi kuwa jaji wa mahakama ya juu nchini.

 Akizungumza katika hafla ya kumkaribisha iliyofanywa na tume ya huduma za mahakama JSC, jaji Koome ameahidi kushirikiana na wenzake katika mahakama hiyo ili kutumiza matarajio ya wakenya katika kutenda haki.

Siku ya jumatano rais Uhuru Kenyatta alimuidhisha Jaji Koome kuw ajaji mkuu mpya nchini na kuchapisha jina lake katika gazeti rasmi la serikali.

Jaji Koome mwenye umri wa miaka 61 ana tajriba ya kazi ya uanasheria kwa zaidi ya miaka 30.

BY Warda Ahmed