HabariSiasa

KIONGOZI WA CHAMA CHA ANC MUSALIA MUDAVADI AWATAKA WAKENYA KUUNGANA KATIKA JUHUDI ZA KUENDELEZA MAENDELEO.

Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi amewataka wakenya kuungana katika juhudi za kuendeleza maendeleo, huku akiwahimiza kupinga siasa za kejeli ambazo kwa muda mrefu zimeirudisha taifa nyuma Akizungumza kwenye mkutano na wabunge wa zamani wa kaunti ya Murang’a , Mudavadi amewataka wakenya kuwahoji kwa makini viongozi ambao watawachagua kwenye uchaguzi wa mwaka 2022.Mudavadi ambaye alikuwa ameandamana na Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja na yule wa Kakamega Cleopus Malala, aidha wameihimiza umuhimu wa kutataua mambo yanayowaathiri vijana kupitia mazungumzo na mashauriano.Mkutano huu unajiri wiki moja tu baada ya kiongozi huyo kukutana na viongozi wengine wa mlima Kenya uliofanyika Kaunti ya Nyeri.

 

BY JOYCE MWENDWA