Habari

Bibilia iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kidigo yazinduliwa Kwale…

Shirika la Bible Translation & Literacy (BTL) limezindua rasmi Biblia iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kidigo katika kaunti ya Kwale.

Mkurugenzi wa shirika hilo nchini Kasisi Peter Muguti amesema kuwa tafsiri ya Biblia hiyo imechukua miaka 34 kwa gharama ya shilingi milioni 3.5 kuchapishwa.

Akizungumza na wanahabari mjini Kwale, Muguti amesema kwamba wanalenga kutafsiri Biblia za makabila mengine yanayoishi eneo la Pwani.

Kwa upande wake waziri wa elimu kaunti ya Kwale Mangale Chiforomodo amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuboresha viwango vya masomo kaunti hiyo.

Naye Sheikh Kassim Zani amelipongeza shirika hilo kwa hatua hiyo inayolenga kuiunganisha dini ya kiislamu na ile ya kikristo.

By Kwale correspondent