Habari

Familia ya marehemu Bashir Mohamud yasubiri kwa hamu ripoti ya upasuaji……..

Familia ya raia wa Marekani Bashir Mohammed Mahamud inasubiri kwa hamu ripoti ya upasuaji ya mwili wa marehemu kabla ya mazishi baadae leo katika makaburi ya waislamu ya Langata jijini Nairobi.

Mwanapatholojia mkuu wa serikali Johansen Oduor anatarajiwa kuongoza shughuli hiyo ya upasuaji na kuweka wazi ripoti ya kilichosababisha kifo chake, baada ya kuripotiwa kutoweka wiki mbili zilizopita.

Mwili wa marehemu ulipatikana katika mto Nyamindi kaunti ya Kirinyaga tarehe 16 mwezi huu siku tatu tuu baada ya kuripotiwa kutoweka , na mara ya mwisho kuonekana katika mkahawa mmoja eneo la Lavington.

Gari lake lilipatikana huko Ngong likiwa limeteketezwa.

Inaarifiwa kwamba mwili wake ulikuwa na alama za kukatwa na pia risasi.

By Nick Waita