Habari

MAAFISA WAWILI WA POLISI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA SABA JELA………

Maafisa wawili wa polisi William Chirchir na Godfrey Kirui wamehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kupatikana na hatia ya kumuua mwanamke katika bustani ya City jijini Nairobi.

mauaji haya yalitekelezwa tarehe 20 mwezi mei mwaka 2018.

Tarehe 11 mwezi huu wawili hao walipatikana na hatia ya kumuua mfanyibiashara Janet Waiyaki kwa kumpiga risasi akiwa ndani ya gari pamoja na mwanamume ambaye pia alijeruhiwa kwa risasi katika bustani ya City.

Jaji Stella Mutuku aliwapata wawili hao kwa hatia ya mauaji huku akisema hawakustahili kutumia nguvu kuwakabili wawili hao ambao hawakuwa tishio kwao.

BY JOYCE MWENDWA