HabariNews

Waziri Magoha apiga mikutano yoyote shuleni

Waziri wa elimu prof. George Magoha amepiga marufuku kuandaliwa kwa mikutano yoyote shuleni.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Magoha amesema kuna baadhi ya watu na vikundi ambavyo vina mazoea ya kuandaa mikutano hasa ya kisiasa katika shule mbalimbali humu nchini, jambo ambalo linawaweka wanafunzi katika athari ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Magoha aidha amesema wizara ya elimu itamchukulia hatua kali yeyote atakayejaribu kuandaa mkutano katika shule za humu nchini

 

By Joyce Mwendwa