AfyaMakala

Ufahamu Ugonjwa Wa Amenorrhea (Ukosefu Wa Hedhi) na chanzo chake…………….

Huu ni ugonjwa unaosababisha wnawake kukosa siku zake za mwezi yaa Hedhi hali inayopelekea usumbufu mwingi wa kisaikolojia .Tatizo la kukosa hedhi au kitaalamu amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa  au baadaye kabisa maishani.Primary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kubalehe kama vile kuota matiti, au msichana anaweza kuwa na mabadiliko ya kubalehe lakini asipate hedhi.Vile vile Tatizo hilo linapotokea baadaye kitaalamu huitwa Secondary amenorrhea, hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito, hanyonyeshi na ambaye hajavuka umri wa kukosa hedhi kitaalamu menopause na wala hatumii njia za kupanga uzazi kama vile sindano au vidonge na ambaye hapo awali alikuwa akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa miezi mitatu au zaidi.Ili mwanamke aweze kuwa na mzunguko ulio sahihi wa hedhi, ni lazima matezi yake (ya hypothalamus na pituitary) pamoja na kiwanda cha kutengeneza mayai ya kike (ovaries) na mji wa mimba (uterus) vifanye kazi zake sawasawa.Hypothalamus huchochea tezi la pituitary kuzalisha homoni chochezi ya follicle au follicle-stimulating hormone (FSH) pamoja na homoni ya luteinizing (LH). Hizi FSH na LH kwa pamoja huchochea ovaries kuzalisha homoni za estrogen pamoja na progesterone.Kazi za estrogen na progesterone ni kusababisha mabadiliko katika ukuta wa uterus yaani endometrium ikiwepo kupata hedhi.

 

By Yussuf Tsuma