Habari

Serikali ya Kwale yatenga makadirio ya bajeti…..

Serikali ya kaunti ya Kwale kupitia wizara ya fedha imetenga makadirio ya bajeti ya takriban shilingi bilioni 9.8 katika mwaka wa kifedha wa 2021/2022.

Waziri wa fedha kaunti hiyo Bakari Sebe amesema kuwa bajeti hiyo itaanza kutelekezwa baada ya bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2020/2021 kukamilika mwezi huu.

Haya yanajiri huku waziri wa fedha Ukur Yattani akitarajiwa kusoma bajeti ya shilingi trilioni 3.6 ya mwaka wa kifedha wa 2021/2022 itakayotekelezwa kuanzia mwezi ujao.

Waziri huyo amebainisha kwamba idara za afya na elimu zimepewa kipaumbele katika bajeti hiyo ya kaunti ya Kwale.

Sebe ameeleza kuwa wizara ya afya imetengewa shilingi bilioni 3 kutokana na janga la corona huku wizara ya elimu ikipata shilingi bilioni 1.5 kaunti hiyo.

 

Kwale Correspondent