HabariMakala

Ukosefu wa vyeti vya Ndoa Taita wawanyima bima za matibabu wanandoa……..

Ukosefu wa vyeti vya ndoa katika kaunti ya Taita Taveta, umetajwa kuwa mojawapo ya changamoto kwa wakaazi kukosa kujiandikisha katika bima ya matibabu.

Kulingana na wakaazi ni kuwa kwa muda sasa imekuwa ni vigumu kupata bima ya matibabu kwani wengi wanaoishi kama mume na mke bado hawana pia vitambulisho vya kitaifa.

Haya yanajiri huku zoezi la kujiandikisha kwa utoaji wa bima kupitia mfumo wa kidijitali ukiendelea kaunti hiyo.

 

By Joyce Kelly