Habari

NAIBU WA RAIS AMKASHIFU RAIS UHURU KENYATTA NA KIONGOZI WA ODM RAILA ODINGA

Naibu wa rais Dr wiliium Ruto amekashifu vikali rais uhuru Kenyatta pamoja na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kwa kutumia nguvu ili kubadilisha katiba kwa maslahi yao wenyewe.

Akizungumza nyumbani kwake eneo la Karen kaunti ya Nairobi ruto amesema kwamba katiba ya taifa inapaswa kuheshemiwa na sio kutumika katika kuangazia agenda ya watu binafsi kama inavyoonekana  kwa rais kenyatta na mwenzake raila odinga ambao nia yao ni kubadilisha katiba ili kuweza kujitafutia nafasi.

Ruto aidha ametoa wito kwa viongozi hao kuheshimu katiba kwani wamepewa nafasi hiyo na wananchi wala sio kuangazia maslahi yao na kufanya mwananchi kuzidi kuwa mnyonge.

BY DAVID OTIENO