Habari

Atwoli awalaani walioteketeza ishara ya barabara yenye jina lake……..

Katibu mkuu wa chama cha wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli amesema kamwe hatishiwi wala hababaishwi kufuatia hatua ya ishara ya barabara yenye jina lake kuteketezwa Mtaani Kileleshwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo,hili likiwa ni jaribio la tatu la kuondoa kibao hicho.

Kupitia taarifa yake kwenye ukurasa wa Twitter, Atwoli amesema jina lake linatambulika ulimwengu mzima bila ya kuwepo kwa bango hilo huku akimkemea aliyechukua hatua hiyo kwa kuvunja sheria.

Amesisitiza kwamba bango hilo liliwekwa kisheria na serikali ya kaunti ya Nairobi kwa heshima yake, na juhudi zake za kuwatetea wafanyikazi nchini na kote duniani.

 

BY NEWS DESK