AfyaHabariNews

Wizara ya Afya katika kaunti ya Taita Taveta imeshirikiana na Global Fund kusambaza vyandarua 233,191…

Wizara ya Afya katika kaunti ya Taita Taveta imeshirikiana na Global Fund kusambaza vyandarua 233,191 vya kuzuia mbu kwa wakazi wa Kaunti ya Taita Taveta katika juhudi za kupambana na malaria.

Usambazaji wa neti hizo za bure unalenga watu 381,583 na jumla ya nyumba 87,862 katika kaunti hiyo.

Waliopewa kipaumbele ni pamoja na wachimbaji migodi, wale wanaoishi katika ardhi zenye maji maji, wanaoishi ndani na karibu na mashamba ya ufugaji ili kujizuia kutokana na maambukizi yanayosababishwa na mbu.

BY NICK WAITA