Habari

Uhaba wa madarasa washuhudiwa katika eneo bunge la GANZE…….

Uhaba wa madarasa unaendelea kushuhudiwa katika eneo bunge la Ganze  kaunti ya kilifi huku madarasa mengine yakiwa katika hali duni.

Kwa mujibu wa mbunge wa eneo hilo Teddy Mwambire, eneo bunge lake linahitaji jumla ya shilingi bilioni mbili ili kuweka miundo msingi bora na kuimarisha hadhi ya shule katika eneo bunge la Ganze.

Teddy anasema kwamba shule nyingi katika eneo hilo zimebuniwa na wazazi wa Ganze huku ikidaiwa kwamba nyingi ya shule hizo zimejengwa kwa kutumia matope.

Aidha Mwambire pia amelalamikia uvamizi wa ndovu ambao wamekuwa kero wa wakaazi wa eneo hilo pia kuhatarisha maisha ya wanafunzi wanaoenda shule za kutwa.

 

By Nicky Waita