HabariNews

IEBC yasisitiza kwamba lazima uwe na shahada ili kuwania wadhfa wa kisiasa…….

Tume ya uchaguzi nchini IEBC imesisitiza kwamba watakaolenga kuwania nyadhfa mbali mbali za siasa katika uchaguzi mkuu ujao sharti wawe na shahada.

IEBC imevishauri vyama vya kisiasa kuhakikisha kwamba wagombea wote watakaopewa tiketi wamehitimu.

Akiwasilisha ripoti kuhusu utayari wa tume hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema vyeti vyote vya elimu vitakavyowasilishwa vitatathminiwa kulingana na sehemu ya 47 ya katiba kabla ya kuwapa idhini wagombea.

Chebukati aidha ameiambia kamati ya bunge kuhusu sheria kwamba, IEBC imeanza mchakato wa marekebisho ya sheria za uchaguzi ikiwemo taasisi zilizo na data hazishirikiani na tume hiyo ili kukabili utumiaji wa vyeti ghushi.

Miongoni mwa taasisi hizo ni tume ya elimu ya juu, tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC,idara ya polisi na idara ya mahakama.

Tayari mjadala kuhusu sheria hiyo ungali unaendelea huku bunge la kitaifa likitarajiwa kujadili baadhi ya mapendekezo yanayotaka sheria hiyo iahirishwe au iondolewe.

By Warda Ahmed