AfyaHabariNews

Kagwe asema ana imani ya kumaliza ugonjwa wa malaria nchini………

Waziri wa afya mutahi kagwe ameweka Imani yake katika kumaliza ugoinjwa wa malaria nchini…..

Akizungumza katika uzinduzi wa mipango ya kukabiliana na ugonjwa wa malaria wa mwaka 2021/2025 katika eneo la maziwa makuu kati ya jumuia ya afrika mashariki EAC na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo,Kagwe amesema kwamba ugonjwa wa malaria umesalia kuwa janga katika ya jamii ya Afrika mashariki na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo zikichangia kwa asilimia 25 ya visa vya maambukizi na asilimia 10 ya vifo ulimwenguni.

Kagwe amesema kwamba taifa limepiga hatua katika vita dhidi ya ugonjwa wa malaria eneo la ukanda wa maziwa makuu kwa kinga na matibabu kupitia kwa dawa, kusambazwa kwa vyandarua vya kukinga mbu na kupulizwa kwa dawa ya kuuwa wadudu zimechangia katika kupungua kwa ugonjwa huo.

Mataifa 11 yametangazwa kuwa mataifa ambayo hayana ugonjwa wa Malaria 2 yakiwa ya Bara Afrika nayo ni Morocco  mnamo mwaka 2010 na Algeria mwaka 2009.

By Joyce Mwendwa