HabariSiasa

RAIS KENYATTA AWASILI PARIS…………

Picha Kwa Hisani ya PSCU

Rais Uhuru Kenyatta amewasili nchini Paris,Ufaransa  kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini humo.

Rais Kenyatta aliondoka humu nchni jana jioni na anatarajiwa kutia saini mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa barabara kuu kutoka Nairobi hadi mau itakayogharimu  shilingi bilioni 160 na  unaotarajiwa kuanza mwezi Septemba.

Mpango huu utasaidia kupunguza msongamano kwenye ukanda wa kaskazini.

Mradi huu pia unalenga kupanuka kwa barabara ya Rironi- Mai Mahiu–Naivasha, ujenzi wa barabara kuu yenye urefu wa kilomita nne kupitia mji wa Nakuru.

 

BY NICK WAITA