AfyaHabari

SERIKALI KUPANUA UWEZO WA KUHIDAFHI DAMU

Serikali imepanga  kupanua uwezo wa kuhifadhi damu  kutoka panti  20,500  hadi  panti 49,500 kufika mwisho wa mwezi huu.

Vyumba vitatu vya  baridi katika benki za mkoa kwa sasa ziko katika ukarabati kama njia moja ya kukaba upungufu wa damu nchini ,ambayo imeona kuongezeka kwa kasi rufaa za mchango wa damu.

Wizara ya afya imetoa vyumba vitatu baridi vya kuhifadhi damu vilevile majokofu 8 hatua  ambayo inatarajiwa kuenda mbali katika kuhakikisha kuwa hakuna mgonjwa yeyote atakaye kosa damu nchini.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amehimiza kaunti zisizo na taasisi za damu  kuanzisha kwa masaada kutoka  huduma za kitaifa za kuhifadhi  damu.

 

BY NATASHA SAGHE