HabariNews

SERIKALI ZA KAUNTI ZATAKIWA KUWAAJIRI MADAKTARI WA KIKE WA UPASUAJI WA MAITI…

Serikali za kaunti zimetakiwa kuwaajiri madaktari wa kike wa upasuaji wa maiti ya wanawake wa dini ya kiislamu.

Akizungumza katika kaunti ya Kwale,mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji amesema kuwa uajiri wa madaktari hao utafanikisha upasuaji wa maiti hiyo kuambatana na dini ya kiislamu.

Haji amedokeza kwamba hatua hiyo ni mikakati ya serikali ya kuhakikisha waathiriwa wa kesi za mauaji wanapata haki mahakamani.

Kwa upande wao viongozi wa kidini wameshinikiza mikakati ya upasuaji wa maiti kufanyika kulingana na sheria za dini hiyo.

Wakiongozwa na sheikh Rajab Ramadhan, viongozi hao wametaka upasuaji huo kufanyika haraka kabla ya maiti hiyo kuzikwa.

BY BINTIKHAMIS MOHAMMED