Kimataifa

HAITI YAOMBA VIKOSI VYA USALAMA BAADA YA MAUWAJI YA RAIS JOVENEL

Haiti imeomba vikosi vya kigeni kupelekwa nchini humo kulinda miundo mbinu muhimu baada ya kuuawa kwa Rais Jovenel Moïse.

 

Ombi hilo lilitumwa kwa serikali ya Marekani na Umoja wa Mataifa (UN), lakini Marekani imesema haina mpango wakutoa msaada wa kijeshi “wakati huu”.

 

Awali polisi wa Haiti walisema kundi la mamluki 28 wa kigeni walihusika na mauaji ya rais siku ya Jumatano.

 

Baada ya makabiliano makali ya bunduki katika mji mkuu wa Port-au-Prince, 17 kati yao walikamatwa.

 

By KHADIJA BINTI MZEE