HabariNewsSiasa

WANAFUNZI WALIOPATA ALAMA YA 350 NA ZAIDI KUDHAMINIWA KAUNTI YA KWALE …

Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya amesema kuwa wanafunzi wote wa shule ya msingi waliofanikiwa kupata alama ya 350 na zaidi katika mtihani wa kitaifa wa KCPE watadhaminiwa na serikali ya kaunti hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kuwatawaza wanafunzi waliopita mtihani huo katika shule ya msingi ya Kituoni eno la samburu Chengoni, Mvurya amesema kuwa wanafunzi hao watapata mafunzo ya bure hadi wakamilishe shule ya sekondari kwa kuwa watapokea msaada kutoka kwa serikali ya kaunti hiyo.

BY CAROLINE NYAKIO