Habari

Wahudumu Wa Boda boda Kaunti Ya Mombasa wahimizwa kuwekeza kwenye hazina ya NSSF………..

Wito umetolewa kwa wahudumu wa Bodaboda Katika Kaunti ya Mombasa kuwekeza katika hazina ya NSSF ili wanufaike na maisha ya baadae.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Serikali Kanali Mstaafu Cyrus Oguna ni kwamba wahudumu wa Boda boda wamechangia pakubwa kwa pato la Taifa hili na ni lazima wajiwekee hazina hiyo ili kuwafaa baada ya kustaafu kufanya biashara hiyo.

Wakati uo huo Oguna amewahimiza wahudumu katika sekta hiyo kushirikiana na kuhakikisha kwamba wanachangia katika hazina ya matibabu ya NHIF ili kupata huduma za afya bila changamoto zozote.

Katika kikao hicho ambacho kiliwaleta pamoja wahudumu katika ukumbi wa Tononoka mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha wahudumu wa boda boda Kelvin Mubadi amewahimiza umuhimu wa kujiwekea akiba.