Habari

Shughuli ya ukarabati wa barabara ya kutoka Bamburi kuelekea Shanzu zaanza rasmi……..

Shughuli ya ukarabati wa barabara ya kutoka Bamburi kuelekea Shanzu imeanza na itagharimu mtozwa ushuru shilingi milioni 100.

Kukamilika kwa barabara hiyo kutahimarisha miundo misingi pamoja na kukabiliana na swala la mafuriko wakati wa mvua.

Wakizungumza katika hafla ya uzinduzi  wenyeji hasa madereva wa bodaboda na wanawake wamesisitiza kuwa swala la usalama litaimarika kutokana na msitu wa Bamburi ulioko karibu.

Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo amemtaka mwanakandarasi kuwaajiri vijana wa eneo hilo huku wenyeji wakitazamia kuwa matatizo ya wanawake kujifungua kwenye barabara na usalama utaboreka.