AfyaHabari

WATU WENYE AKILI TAAHIRA KATIKA KAUNTI YA MOMBASA KUPIMWA.

Huku serikali ikiendelea kujizatiti kukabili maambukizi ya virusi vya corona, shirika la kijamii la Mombasa Women Empowerment Network limetangaza rasmi mpango wa kuwapima baadhi ya watu wenye akili taahira katika kaunti hii ya Mombasa.

Kiongozi wa shirika hilo Amina Abdalla amesema wataendesha shughuli hiyo katika mitaa mbali mbali kaunti ya Mombasa.

Tangu janga la corona kuripotiwa humu nchini, jumla ya watu 120 wenye akili taahira wamepimwa virusi hivyo.

Baadhi ya watu hao walipatikana wameambukizwa huku hali yao ya afya ikiendelea kuwa mbaya.

 

 BY REPORTER