HabariNews

Zaidi ya wanafunzi elfu 200 waliofanya KCSE wasajiliwa katika vyuo vikuu vya umma…….

Wanafunzi 265,145 waliofanya mtihani wa KCSE wamesajiliwa kwenye vyuo vikuu vya umma na vyuo vya kiufundi katika mwaka wa masomo wa 2021/2022

137,072 kati yao watafanya kozi mbalimbali katika vyuo vya kiufundi maarafu kama TVET huku 128,073 wakisajiliwa kwenye vyuo vikuu nchini.

Hata hivyo idadi ya wanafunzi waliofuzu kufanya diploma imeongezeka kutoka kwa 146,193 mwaka wa 2019 hadi 193,949 mwaka wa 2020 hii ikiwa ni asilimia 33

Waziri wa elimu nprof George Magoha amewataka walimu na wazazi kuwashauri wanafunzi kuhusu kozi zinazoambatana na uwezo wao.

Wanafunzi wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne wanaweza kujua chuo kikuu watakachojiunga nacho kupitia ujume mfupi kwa kutuma maelezo yao kwa 2084.

By Joyce Kelly