HabariNews

Serikali yatakiwa kuweka adhabu kali kuwakabili wanaofanya dhulma za kijinsia…….

Shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika limeitaka serikali kuhakikisha kuwa imeweka adhabu kali dhidi ya wale wote ambao wanaendeleza dhulma za kijinsia nchini.

Kulingana na naibu mkurugenzi katika shirika hilo Salma Hemed bado kuna visa vingi vya dhulma za kijinsia haswa wakati huu ambapo taifa linaendelea kukabiliana na janga la korona na kuitaka idara ya mahakama kuhakikisha washukiwa wote wanakabiliana kisheria.

Kulingana na Hemed wanawake wengi wanalalamikia hali ya wanaume kuwadhulumu jambo ambalo wanasema linachangiwa na kukosa mapato yao ya kila siku.

By Gladys Marura