HabariNewsSiasa

Baadhi ya viongozi waliokuwa wakiunga mkono ripoti ya BBI tayari wamekubali uamuzi huo…

Huku mchakato wa ripoti ya kubadili katika BBI ikizimwa kufuatia uamuzi wa mahakama hapo jana baadhi ya viongozi waliokuwa wakiunga mkono ripoti hio tayari wamekubali uamuzi huo.

Akizungumza na wanahabari hapa Mombasa Mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji aliyepia mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amesema tayari idara ya mahakama ishatoa uamuzi wake wa mwisho na kama mjumbe na mwanachama wa chama cha ODM anakubali uamuzi huo na kuwa anakubaliana na kauli ya kinara wa chama hicho cha ODM Raila Odinga kusema anakubaliana na uamuzi huo na sasa ni wakati wa kusonga mbele na kuangalia masuala ya kujenga taifa.

Kadhalika amesema anakubali juhudi za idara ya mahakama katika mchakato mzima wa kushughulikia na kujadili ripoti hiyo kwa kina hatimae kuizima licha ya kuwa ripoti hiyo ilitiwa sahihi na wajumbe wengi.

Aidha amesema mkenya yoyote ambaye atakuwa na wasiwasi na uamuzi huo wa mahakama kuu anayo haki ya kikatiba kuenda kwa mahakama ya upeo kuitetea ila wao kama chama cha ODM washakubali uamuzi wa mahakama.

Hata hivyo ripoti hio ilizimwa kwa kuwa ilikiuka sheria za katiba ya Kenya.

BY NEWS DESK