HabariNewsSiasa

WAZIRI FRED MATIANG’I KUFIKA MBELE YA KAMATI YA UTAWALA HII LEO…

Waziri wa usalama wa ndani dkt Fred Matiangi ameagizwa kufika mbele ya kamati ya utawala na usalama ya bunge la kitaifa hapo kesho kutoa mwangaza juu ya kuondolewa kwa maafisa wa GSU waliokuwa wakimlinda naibu wa rais William Ruto.

Katika barua ya karani wa bunge Michael Siyalai, Matiang’I ametakiwa kufika mbele ya kamati hiyo pamoja na inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai.

Siyalai amesema kutolewa kwa maafisa wa GSU waliokuwa wakimlinda Ruto ni jambo linalohusu usalama wa kitaifa na ni lazma lishuhulikiwe.

Haya yanajiri huku naibu rais William Ruto akipuuzilia mbali hatua hio na kuwataka wakenya kutopoteza muda mwingi kujadili swala hilo.

Naibu wa rais amelitanga bunge kuelekeza juhudi zake katika kuhakikisha kwamba maafisa wa kutosha wa usalama wanatumwa katika maeneo ambayo visa vya uhalifu vimekithiri.

Ikumbukwe swala hilo lilitarajiwa kuzungumziwa katika bunge la seneti kufuatia wito wa seneta wa Nandi Simon Cherargei.

BY NEWS DESK