AfyaHabariNews

Wauguzi Mombasa watishia kusitisha huduma kuanzia jumatatu wiki ijayo…..

Wauguzi na maafisa wa kliniki kaunti ya Mombasa wametishia kuandaa mgomo baridi kuanzia jumatatu wiki ijayo kufuatia kucheleweshwa kwa mishahara yao.

Wakiongozwa na katibu wa wauguzi hao tawi la Mombasa Peter Maroko, anasema kwa miezi miwili sasa serikali ya kaunti bado haijawalipa mishahara yao jambo ambalo linatatiza maisha yao ya kila siku.

Anasema licha ya wao kutafuta muafaka katika afisi husika kuhusu kuchelewa kwa mshahara wao bado hawajapata suluhu.

Kwa upande wake katibu wa muungano wa matabibu Frankline Makanga anasema kando na mshahara wao wa miezi miwili kucheleweshwa pia pesa wanazokatwa kulipiwa huduma mbali mbali za serikali bado hazijawekwa kwenye akaunti husika kwa miiezi mitano sasa, suala linalowafanya kukosa huduma hizo muhimu.

Wahudumu hao wa afya sasa wamesisitiza kwamba hawalegeza msimamo wao hadi maslahi yao yazingatiwe kikamilifu huku wakihimiza wananchi kutafuta huduma mbadala ifikapo jumatatu wiki ijayo.

BY NEWS DESK