HabariKimataifaSiasa

Mudavadi amshauri Ruto kujiuzulu iwapo haridhiki na utenda kazi wa rais Uhuru Kenyatta……

Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi ndiye kiongozi wa hivi punde kuzungumzia tofauti inayoshuhudiwa baina ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Rutto.

Akihojiwa na kituo kimoja cha redio humu nchini mapema leo, Mudavadi amemshauri Ruto kujiuzulu iwapo haridhiki na utenda kazi wa rais Uhuru Kenyatta.

Wakati huo huo, Mudavadi amewaonya wasiasa dhidi ya kulumbana hadharani kuhusiana na uchaguzi mkuu ujao hususan katika sehemu za ibada.

BY NEWS DESK